Siku kama ya leo miaka
16 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 28 Mei 1998, kwa mara ya kwanza
Pakistan ilianza kufanya majaribio matano ya makombora ya nyuklia.
Majaribio hayo yalifanyika zikiwa zimepita wiki mbili tu, tokea mahasimu
wao yaani India kufanya majaribio yao ya kombora la nyuklia. Baada ya
hapo nchi hizo mbili zilikuwa zikipokezana katika kufanya majaribio yao
ya makombora ya nyuklia. Amma cha kushangaza ni kuwa, majaribio ya
nyuklia ya Pakistan yamekuwa yakizikasirisha mno nchi za Magharibi za
Marekani na Ulaya, na kufikia hatua ya kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya
kiuchumi.
---------------------------------------------------------------------------------------------
Siku kama ya leo miaka 74
iliyopita inayosadifiana na tarehe 28 Mei 1940, Ubelgiji ambayo
ilitangaza kutoegemea upande wowote mwanzoni mwa Vita Vikuu vya Pili vya
Dunia, ilitekwa na majeshi ya Kinazi ya Ujerumani. Majeshi ya Ubelgiji
ambayo yalikuwa yakipata usaidizi wa Uingereza, yalisimamisha vita
kutokana na amri ya Mfalme Leopold wa Tatu, licha ya kusimama kidete kwa
muda wa siku 18 dhidi ya majeshi ya Kinazi ya Ujerumani. Hatua hiyo ya
mfalme Leopold, iliwakasirisha mno wananchi wa Ubelgiji na kuandaa
mazingira ya kuondolewa kwake madarakani mwaka 1951.
Na Siku kama ya leo miaka 98
iliyopita, inayosadiana na tarahe 28 Rajab 1337 Hijria, alifariki dunia
Ayatullahil Udhma Muhammad Kadhim Tabatabai Yazdi maarufu kwa jina la
Allamah Yazdi, msomi mashuhuri wa Kiirani. Allamah Yazdi alijipatia
elimu yake ya kidini ndani na huko Najaf nchini Iraq, kutoka kwa
maulamaa kadhaa mashuhuri akiwemo Mirzai Shirazi na hatimaye kufikia
daraja ya Ijtihad. Msomi huyo aliandika vitabu vingi, kikiwemo kitabu
cha 'al U'rwatul Wuthqa.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!