Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, watoto 200
000 walio chini ya umri wa miaka 5 nchini Somalia wanakabiliwa na
hatari ya kupoteza maisha kutokana na lishe duni na umetoa wito wa
kupelekwa misaada ya dharura ili kuepusha hali hiyo.
Maafisa waandamizi wa UNICEF wamesema kufikia mwishoni mwa mwaka huu maafa makubwa ya watoto yanaweza kushuhudiwa huko Somalia iwapo misaada ya dharura ya chakula na dawa haitapatikana. Msemaji wa Shirika hilo la UN, Christophe Boulierac amesema Somalia inakabiliwa na ukame jambo linalohatarisha mustakabali wa watoto hao. Tahadhari hiyo ya UNICEF imetolewa katika hali ambayo, wanamgambo wa al-Shabab wameanza kujipanga upya na katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kushangaza katika maeneo nyeti ya serikali katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Kuongezeka hali ya ukosefu wa usalama nchini Somalia kumekuwa kukiathiri shughuli za utoaji misaada kwa raia wa nchi hiyo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!