Rais Barack Obama wa Marekani
ametangaza kile alichosema ni ramani ya njia ya kuondoka majeshi ya nchi
yake huko Afghanistan. Kwa mujibu wa mpango huo, Marekani itabakisha
takriban wanajeshi 10 000 nchini Afghanistan badala ya kuondoa kikosi
chote kufikia mwishoni mwa mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa na
kukubaliwa huko nyuma.
Kiongozi huyo amesema wanajeshi hao watakuwa na
jukumu la kutoa mafunzo zaidi kwa wanajeshi wa Afghanistan na kwamba
shughuli zao zitajikita zaidi katika mji mkuu, Kabul na katika kituo cha
kijeshi cha Bagram.
Hata hivyo, yote hayo yatategemea iwapo
rais atakayechaguliwa Afghanistan atakubali kusaini makubaliano ya aina
hiyo. Wachambuzi wengi wanaamini kwamba, rais mpya ajaye nchini
Afghanistan yumkini akakubali kusaini makubaliano ya kuruhusu Washington
kubakisha maelfu ya wanajeshi katika nchi hiyo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!