Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » JE,ULIKUWA UNAZIFAHAMU HIZI HISTORIA ZINAZO AMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO YA IJUMAA YA MEI 30 MWAKA 2014?

JE,ULIKUWA UNAZIFAHAMU HIZI HISTORIA ZINAZO AMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO YA IJUMAA YA MEI 30 MWAKA 2014?

Written By Unknown on Friday, 30 May 2014 | Friday, May 30, 2014

Leo ni tarehe Mosi mwezi wa Shaaban. Mwezi wa Shaaban ni mwezi wa ibada, kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kuomba maghfira. Mtume Muhammad (SAW) aliutukuza mno mwezi huu na kuuita kuwa ni mwezi wake. Mtume Mtukufu na Maimamu watoharifu waliusia mno kufanya ibada hasa kufunga katika mwezi huu wa Shaabani kwa sababu ndio unaotayarisha uwanja mzuri wa kuingia kwenye mwezi wenye baraka tele wa Ramadhani. Mambo mengi muhimu yamejiri katika mwezi huu wa Shaaban, kama kuzaliwa Imam Hussein bin Ali (as) mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad (SAW) na pia tukio la kuzaliwa Imam wa zama, Mahdi Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake. Wote wanamsubiri Mahdi arejee ili uadilifu uweze kuenea duniani. Ni matumaini yetu kuwa sote tutajitahidi kunufaika na fursa adhimu zilizopo katika mwezi huu uliojaa baraka.

          ---------------------------------------------------------------------------

Siku kama ya leo miaka 236 iliyopita sawa na tarehe 30 Mei 1778, Francois - Marie Arouet maarufu kwa jina la Voltaire, mwanafalsafa na mwandishi wa Kifaransa alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 84. Katika maisha yake, Voltaire aliwahi kuwekwa mahabusu mara mbili na kubadilishwa kwa muda wa miaka mitatu nchini Uingereza. Kitendo hicho kilimkasirisha sana Voltaire na kumfanya kuwa dhidi ya utawala wa Ufaransa.
 
          ---------------------------------------------------------------------------

Siku kama ya leo 90 miaka iliyopita, alifariki dunia Ali Akbar Khan Nafisi aliyejulikana kama Naadhimul Atwiba, daktari na mtaalamu wa lugha wa Kiirani, katika mji wa Tehran. Baada ya kumaliza masomo yake ya mwanzo alianza kujifunza masomo ya kidini na pia udaktari katika chuo cha Darul Funun cha Tehran. Baadhi ya vitabu vilivyoandikwa na Naadhimul Atwiba katika uwanja wa tiba vimetarjumiwa katika lugha za kigeni. Ali Akbar Khan Nafisi ambaye pia alikuwa mtaalamu wa lugha alifanya jitihada nyingi katika kukusanya maneno ya lugha ya Kifarsi na kuandika kamusi inayoitwa 'Kamusi ya Nafisi.'
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi