Rais Joyce Banda wa Malawi amesema kuwa yupo tayari kuondoka
madarakani iwapo mahakama kuu ya nchi hiyo itaamua hivyo kuhusu mgogoro
wa uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita na mpinzani wake kutangazwa
mshindi. Hata hivyo Bi. Banda amesema bado anaamini kulitokea
udanganyifu katika uchaguzi huo. Mahakama Kuu ya Malawi inatarajiwa leo
kuamua iwapo Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo (MEC) itangaze matokeo ya
uchaguzi wa Mei 20 ambayo mpinzani wa Banda anatarajiwa kuwa mshindi, au
itoe amri ya kuhesabiwa tena kura, hatua ambayo huenda ikachukua muda
wa miezi miwili. Rais Banda amesema kuwa, atakubali uamuzi utakaotolewa
na mahakama hiyo na kwamba atapumzika siasa akijua kuwa alifanya
jitihada za kulinda haki za Wamalawi katika kipindi nyeti ili
kuhakikisha kuwa wanapata kiongozi aliyechaguliwa kwa njia ya haki na
kuaminika.
Wiki iliyopita Rais Banda alibatilisha uchaguzi mkuu wa rais na kutaka uchaguzi mwengine mpya uitishwe ndani ya muda wa siku 90 akisema kuwa kulitokea udanganyifu na ukiukwaji mkubwa wa kanuni za uchaguzi.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!