Maafisa wa ngazi za juu wa Uturuki wamekataa kuwapa hifadhi
wakimbizi wa Syria ambao wanakimbilia nchini humo. Ahmet Davutoglu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema kuwa, nchi yake inaruhusu
idadi ndogo tu ya wakimbizi wanaotafuta hifadhi kutoka bara Ulaya na kwa
ajili hiyo haiwezekani wakimbizi wa Syria kupewa hifadhi nchini humo.
Hivi sasa wakimbizi ambao hawatoki Ulaya wanapewa kibali cha muda cha kuishi nchini Uturuki, huku wakisubiri kuelekea katika nchi nyingine kutafuta hifadhi.
Hayo yanajiri huku machafuko na mapigano nchini Syria yakisababisha mamilioni ya wananchi wa nchi hiyo wakimbililie nchi jirani ikiwemo Uturuki.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!