Petro Poroshenko rais mteule wa Ukraine ameapa kuwaadhibu waasi
wanaoungwa mkono na Russia ambao wameshambulia helikopya ya jeshi
mashariki mwa nchi hiyo na kuua askari 14 akiwemo jenerali wa jeshi.
Poroshenko amewaita wanamgambo hao wanaotaka kujitenga eneo la mashariki
mwa Ukraine kuwa ni 'magaidi' na 'majambazi'.
Kutunguliwa helikopta hiyo huko Ukraine kumepelekea Marekani iseme kuwa inashuku waasi hao wanasaidiwa kutoka nje na kwamba kuna uthibitisho kuwa kuna watu wanaopewa mafunzo Russia na kuingia Ukraine. Russia imekanusha madai hayo na kuitaka serikali ya Kiev kusitisha mapigano haraka na kuzitaka nchi za Magharibi zizuie kupanuka zaidi mgogoro wa Ukraine.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!