Christine Lagarde Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF)
amesema kuwa uchumi wa nchi za Kiafrika unahitajia uwekezaji wa dola
bilioni 93 kwa mwaka kwa ajili ya kukarabati miundombinu. Sambamba na
kukiri kuwa maendeleo yameshuhudiwa katika eneo la Afrika la chini ya
Jangwa la Sahara katika miaka ya hivi karibuni kwa asilimia 5.5. Lagarde
amesisitiza kuwa miongoni mwa matatizo yanayokabili sekta ya uchumi ya
Afrika pamoja na mambo mengine ni kuchelewa nchi za bara hilo kuimarisha
miundombinu na uzalishaji umeme.
Mkuu huyo wa IMF aidha amesema, miundombinu ya viwango vya juu inaweza kuvutia wawekezaji wa nje katika bara la Afrika. Lagarde alisema hayo katika mkutano ulioanza jana huko mjini Maputo Msumbuji kwa lengo la kujadili changamoto za kiuchumi zinazolikabili eneo la kusini mwa Afrika.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!