Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtaka rais mteule
wa Misri afanye jitihada za kufanya mazungumzo na makundi na mirengo
yote ya nchi hiyo ili kumarisha umoja na mshikamano nchini. Msemaji
wake Stephan Dujaric amesema kuwa, Ban Ki Moon amemtaka Abdulfattah al
Sisi afungue mlango wa mazungumzo na makundi yote ya nchi hiyo ili
kuimarisha amani na kuleta maendeleo na kwamba suala hilo lina umuhimu
mkubwa.
Katika upande mwingine wafuasi wa rais aliyepinduliwa na jeshi nchini Misri Muhammad Mursi wameandamana katika miji tofauti ya nchi hiyo kulalamikia uchaguzi wa rais uliofanyika hivi majuzi nchini humo. Waandamanaji hao sambamba na kutoa nara dhidi ya Abdulfattah al Sisi, jeshi na polisi wamesisitiza kuwa Musri ndiye rais halali wa Misri na kupinga uchaguzi wa hivi karibuni ulioplekea ushindi wa Abdulfattah al Sisi mkuu wa zamani wa jeshi la nchi hiyo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!