Siku kama ya leo miaka 196 iliyopita, alizaliwa Karl
Heinrich Marx mwanafalsafa wa Kijerumani na mwasisi wa nadharia ya
Umaksi. Karl Marx awali alianza kusomea taaluma ya sheria na baadaye
historia na falsafa. Mwanafalsafa huyo wa Kijerumani kwa muda fulani
alikuwa mkuu wa jarida moja na mwaka 1848 alishirikiana na mwanafalsafa
mwenzake wa Kijerumani na kubainisha imani, maoni na mitazamo yake
katika kitabu walichokiandika na kukipa jina la "Manifesto ya
Ukomonisti." Miaka miwili baadaye Marx alibaidishwa kutokana na
kujishughulisha na harakati za kisiasa na hadi mwishoni mwa maisha yake
makazi yake yalikuwa nchini Uingereza.
************************************************************
Siku kama ya leo miaka 193 iliyopita, alifariki dunia
Napoleon Bonaparte mfalme aliyekuwa na nguvu wa Ufaransa, akiwa
uhamishoni. Napoleon alizaliwa mwaka 1769 Miladia na kuchukua madaraka
makubwa ya uongozi baada ya mapinduzi ya Ufaransa mwaka 1789, ambapo
aliifanya nchi hiyo ishinde vita na nchi nyingi za Ulaya. Baada ya kuwa
mfalme wa Ufaransa Napeleon Bonaparte aligeuka kuwa mtawala aliyependa
kujitanua na kuzivamia nchi nyinginezo katika nukta tofauti duniani. Kwa
ajili hiyo katika kipindi cha utawala wake alipigana vita kadhaa na
nchi nyingine na kukalia kwa mabavu maeneo mengi ya bara Ulaya.
************************************************************
Na miaka 1191 iliyopita mwafaka na leo, aliuawa shahidi na
mmoja wa watawala wa Bani Abbas, Abu Yusuf Yaqub ibn Is'haq maarufu kwa
jina la Ibnu Sikkit msomi wa Kiislamu na mtaalamu mkubwa wa lugha.
Alizaliwa katika mji wa Khuzestan unaopatikana kusini magharibi mwa
Iran. Alielekea mjini Baghdad na familia yake na kusoma kwa walimu
wakubwa wa zama hizo. Umaarufu wa Ibnu Sikkit katika elimu ulimpelekea
Mutawakil mmoja wa watawala wa Abbasia kumualika kwa lengo la
kuwafundisha watoto wake. Kwa kuwa Ibnu Sikkit alikuwa na mapenzi
makubwa kwa Watu wa Nyumba ya Mtume (SAW), jambo hilo lilimkasirisha
sana Mutawakkil na kuchukua hatua ya kumuua. Miongoni mwa athari za
msomi huyu ni kitabu kiitwacho "Islahul Mantik."
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!