Uchunguzi wa maoni uliofanyika nchini Afrika Kusini unaonyesha kuwa,
chama tawala cha African National Congress ANC kwa mara nyingine tena
kitajipatia ushindi kwenye uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanyika kesho
kutwa Jumatano nchini humo. Uchunguzi huo wa maoni unaonyesha kuwa,
chama cha ANC kitajipatia ushindi wa zaidi ya asilimia sitini ya kura
zitakazohesabiwa. Uchunguzi huo wa maoni unaonyesha kuwa, chama cha
Muungano wa Demokrasia, chama kikuu cha upinzani nchini humo, kinaweza
kujipatia karibu asilimia 20, kiwango ambacho kinaonekana kuwa kikubwa
kwa chama hicho cha upinzani kikilinganishwa na cha uchaguzi uliofanyika
miaka mitano iliyopita. Chama cha ANC kinashikilia uongozi wa nchi hiyo
tokea ulipoangushwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994. Hivi sasa,
chama cha ANC kinakalia viti 264 kati ya viti 400 katika bunge la Afrika
Kusini. Kwa mujibu wa katiba ya Afrika Kusini, rais wa nchi hiyo
huchaguliwa na wabunge na bila shaka chama kitakachojipatia wingi wa
viti ndicho kitakachoongoza serikali ya nchi hiyo.
Home »
siasa afrika
» KWA MUJIBU WA UCHUNGUZI KUTOKA AFRIKA YA KUSINI WABAINI KUWA HIKI NDICHO CHAMA KITAKACHO SHINDA UCHAGUZI WA WABUNGE NCHINI HUMO
KWA MUJIBU WA UCHUNGUZI KUTOKA AFRIKA YA KUSINI WABAINI KUWA HIKI NDICHO CHAMA KITAKACHO SHINDA UCHAGUZI WA WABUNGE NCHINI HUMO
Written By Unknown on Monday, 5 May 2014 | Monday, May 05, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!