Mwimbaji maarufu wa Pop, Miley Cyrus ambaye alilazwa hospitalini
mwezi uliopita baada ya kusumbuliwa na allergy na flu, amewekwa chini ya
uangalizi mkali wa matabibu.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror, mwimbaji huyo ameruhusiwa kuendelea na ziara yake nchini Uingereza ambayo aliisitisha kwa muda lakini muda wote atakuwa chini ya uangalizi wa matabibu kwa kuwa afya yake hubadilika ghafla na kuishiwa nguvu mara kwa mara.
“Miley amekuwa chini ya matabibu wawili ambao wanaangalia maendeleo yake ya afya masaa 24 akiwa nyumbani. Tayari ameshapewa matabibu ambao watakuwa standby muda wote wakati akiwa kwenye ziara yake ya Uingereza. Kitu kibaya sana ni kwamba ugonjwa wake huwa unatulia kabisa na anakuwa mzima lakini ghafla anaugua tena.” Chanzo kimeliambia gazeti la Daily Mirror.
Imeripotiwa kuwa muda wote alipokuwa hospitalini alikuwa hawezi kula vizuri na kwamba hadi sasa anatumia matunda na mboga za majani ili kuongeza vitamini zaidi mwilini na haruhusiwi kuvuta kitu chochote.
“Sasa hivi anawekwa chini ya uangalizi makini wa chakula na anakula matunda na mboga za majani ili kuongeza vitamin na amezuiwa kutumia vinywaji vikali au kuvuti kitu chochote hususani bangi.” Kimeeleza chanzo hicho

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!