Watu wawili wauwawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa wakati mabomu mawili
yalilipuka ndani ya mabasi ya abiria kwenye barabara kuu kati ya Nairobi
na mji wa Thika. Mwandishi wa sauti ya Amerika anasema mlipuko mmoja
ulitokea karibu na hoteli ya Bluesprings na wa pili ulitokea wakati basi
linapita chini ya daraja ya Kasarani kwenye barabara hiyo ya Thika.
Waathiriwa wamepelekwa kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta na Ruaraka. Na hadi tunapoandika ripoti hii haijajulikana nani aliyehusika, lakini maafisa wa usalama wanadhani ni wanamgambo wa kundi la Kisomali Al-Shabab ndio walohusika.
Mashambulio hayo yametokea muda mchache tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza kwamba zowezi la msako wa usalama linaloendelea nchini humo litaimarishwa kufuatia milipuko miwili iliyotokea Mombasa Jumamosi Usiku.
Rais Kenyatta amelaani mashambulio hayo ya Mombasa na kusema kwamba magaidi watashindwa na watachukuliwa kama wahalifu makatili na hawataweza kuvuruga usalama na utamaduni wa Wakenya kuishi kwa pamoja bila ya kujali misingi ya kidini au kikabila.
Makundi ya kutetea haki za binadamu Kenya yanaitaka serikali kubadili mbinu zake za msako na kuimarisha uwezo wa upelelezi na kushirikiana karibu na wananchi badala ya kupambana nao.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!