Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » KAMA ULIKUWA HAUJUI BASI HIKI NDICHO CHANZO CHA MDOGO WAKE NA BEYONCE KUMTWANGA VIBAO NA MATEKE RAPA JAY-Z

KAMA ULIKUWA HAUJUI BASI HIKI NDICHO CHANZO CHA MDOGO WAKE NA BEYONCE KUMTWANGA VIBAO NA MATEKE RAPA JAY-Z

Written By Unknown on Wednesday, 14 May 2014 | Wednesday, May 14, 2014

Tetesi za chanzo cha mdogo wake Beyonce, Solange kumpiga Jay Z walipokuwa ndani ya lift zinazidi kuzua ripoti kutoka kwa vyanzo mbalimbali.
Kwa mujibu wa The New York Daily News, Solange anadaiwa kuwa alichukizwa na uamuzi wa Jay Z kutaka kuondoka kwenye After Party waliyokuwepo na Beyonce na Solange Standard Hotel na kutaka kwenda kwenye after party ya Rihanna bila Beyonce.

Chanzo kimeiambia Daily News kuwa Solange alimuuliza Jay Z, “kwa nini huendi nyumbani?” na akamuuliza Beyonce pia, “Kwa nini mumeo anataka kwenda club muda huu?” Na Jay Z akajibu “You’re one to talk.”
Inaelezwa kuwa jibu la Jay Z lilichochea kwa kiasi kikubwa hasira za Solange ambaye baadae alizua timbwili la aina yake kwenye lift.
Bado haijathibitishwa chanzo cha Solange kuanza kurusha makofi na mateke kwa Jay Z kwa kuwa katika video iliyosambaa hakuna sauti yoyote inayosikika.
Vyanzo vingine vilieleza kuwa Solange alikuwa amelewa sana wakati wakiwa kwenye after party hiyo na kwamba alizua ugomvi mapema na mgeni mmoja.
Katika hatua nyingine, imeripotiwa kuwa Jay Z na Solange wameonekana wakifanya shopping kwenye duka moja la pete Jumanne, May 13.
Inawezekana wameshamaliza tofauti zao kwa kuwa ugomvi wao ulitokea wiki moja iliyopita licha ya video kusambaa wiki hii.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi