Waziri Mkuu mpya wa Libya ambaye amechaguliwa hivi karibuni
amenusurika kifo baada ya nyumba yake kushambuliwa na watu wenye silaha
hapo jana. Ripoti zinasema kuwa watu wanne walishambulia nyumba ya Ahmed
Maiteg kwa maguruneti, suala lililosababisha utupianaji risasi na
askari usalama. Maiteg aliteuliwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Libya siku
ya Jumatatu.
Hayo yanajiri huku Marekani ikituma manowari ya kivita pamoja na askari wa majini 1,000 katika pwani ya Libya kwenye bahari ya Mediterranean ili kuimarisha kikosi chake ambacho tayari kiko kwenye eneo hilo. Hatua hiyo imetajwa kuwa ni ya tahadhari iwapo hali ya usalama nchini Libya itaendelea kudorora na Marekani kuamua kuwahamisha maafisa wake walioko kwenye ubalozi wa mjini Tripoli. Marekani pia imewataka raia wake kuondoka nchini Libya ambako jenerali mstaafu wa jeshi Khalifa Haftar anafanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo wenye silaha akishirikiana na maafisa wa jeshi walioasi.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!