Muungano wa upinzani wa CORD nchini Kenya unakabiliwa na hatari ya
kusambaratika baada baadhi ya vyama tanzu kuanza kujiondoa kwenye
muungano huo. Chama cha 'The Independent' (TIP) kimetangaza kujiondoa
kwenye muungano huo kwa madai kwamba viongozi wa muungano huo wanatumia
mabavu kuongoza. Kiongozi wa TIP, Kalembe Ndile, ametangaza kuwa, hakuna
uwazi katika muungano huo akidai kuwa unaongozwa na viongozi walafi na
wasiokuwa waaminifu.
Bw Ndile amesema ingawaje chama hicho kiliufanyia kampeni muungano huo katika uchaguzi mkuu uliopita, hakikupata ufadhili wowote baada ya muungano wa CORD kupata sehemu yake ya fedha kutoka kwa hazina kwa ajili ya vyama vya siasa. Kiongozi huyo wa TIP amesemna wanatafuta vyama vingine vyenye fikra na mitazamo sawa waunde muungano huku akiongeza kuwa viongozi waliopo serikalini na upinzani wana mawazo sawa ambayo hayawezi kuleta mabadiliko wanayotafuta Wakenya.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!