Kiongozi wa zamani wa Qatar ameukosoa vikali utendaji wa viongozi wa
hivi sasa wa utawala wa Saudi Arabia na kusisitiza kuwa, watawala wa
Saudia ndio wanaoufedhehesha ulimwengu wa Kiarabu. Sheikh Hamad bin
Khalifa Aal Thani amesema kuwa, watawala wa Saudi Arabia wanakera na
kuzitaka nchi zilizokuwa na mashirikiano mazuri na nchi hiyo zikate
mahusiano yao na serikali ya Riyadh.
Ameongeza kuwa, utawala wa Riyadh utaangushwa katika kipindi cha miaka 12 ijayo, kwani hivi sasa kuna mpasuko mkubwa kati ya Mfalme Abdullah bin Abdulaziz na wanamfalme wa nchi hiyo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi Machi uliopita, nchi za Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain ziliwaita nyumbani mabalozi wao walioko Doha mji mkuu wa Qatar ikiwa ni katika kulalamikia siasa za Qatar za kuiunga mkono harakati ya Ikhwanul Muslimiin ya nchini Misri. Hatua ya serikali ya Qatar ya kumuunga mkono Muhammad Morsi aliyeondolewa madarakani na jeshi la Misri mwaka jana, iliibua hitifalu na mpasuko mkubwa miongoni mwa wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uaje

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!