Beki wa klabu ya Real Madrid anaweza kukosa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Atletico Madrid kutokana na majeruhi yanayomsumbua. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alicheza dakika zote tisini katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Real Valladolid juzi lakini vipimo alivyofanyiwa leo vimebainisha kuwa alipata majeraha ya kigimbi cha mguu wake wa kushoto.
Madrid bado hawajabainisha ukubwa wa tatizo hilo lakini kuna taarifa zinadai kuwa anaweza kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili hatua ambayo inaweka wasiwasi wa kukosekana katika fainali hiyo inayotarajiwa kuchezwa Mei 24 mwaka huu. Cristiano Ronaldo pia alitolewa nje katika mchezo huo dhidi ya Valladolid lakini kocha Carlo Ancelotti haraka aliwaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kudai kuwa hayakuwa majeraha ya kutisha.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!