Siku kama ya leo miaka 1448
iliyopita, Mtume Mtukufu wa Uislamu Muhammad Mustafa SAW alibaathiwa
yaani kupewa Utume na Mwenyezi Mungu. Kipindi hicho Mtume Muhammad SAW
alikuwa amefikisha miaka 40 katika umri wake uliojaa baraka. Mtume
Muhammad SAW alianza kutafakari na kudurusu maumbile ya dunia akiwa bado
mdogo na daima alikuwa akifirikia njia za kunyanyua juu utukufu wa
mwanadamu. Alikuwa maarufu kwa ukweli, uaminifu na kutenda mema. Jumla
ya sifa hizo njema zilimfanya Muhammad SAW kuwa shakhsia mwenye hadhi na
heshima kubwa katika jamii. Alipitisha muda wake mwingi katika ibada na
kutafakari katika Pango la Hiraa kaskazini mwa Makka. Malaika Jibrail
alimteremkia Muhammad akiwa katika pango hilo na kumpa bishara ya kwamba
ameteuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa Mtume wake kwa walimwengu wote. Tangu
siku hiyo Mtukufu huyo alipewa jukumu kubwa la kuongoza wanadamu na
kupambana na ujahili, ukafiri, dhulma na uonevu. Mtandao wako wa habari wa http://www.ismailniyonkuru.info/ unatoa
mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaba wa siku hii adhimu.
Miaka 20 iliyopita katika siku
kama ya leo inayosadifiana na siku ya Ijumaa usiku wa tarehe 27 Rajab
1415 Hijiria, Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
ilianza kurusha matangazo yake kwa mara ya kwanza. Matangazo ya Radio
Tehran yalianza kurushwa kwa muda wa nusu saa tu usiku, na yalifunguliwa
kwa mnasaba wa kuadhimisha siku ya kubaathiwa na kupewa Utume, Bwana
wetu Muhammad (SAW).
Lengo la kuasisiwa Idhaa ya
Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kufikisha sauti ya
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa wananchi wanaodhulumiwa wa bara la
Afrika, kuelimisha na kufichua njama za ubeberu wa kimataifa dhidi ya
bara hilo.
-----------------------------------------------------------------------------
Miaka 104 iliyopita siku kama
leo, aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 67 Robert Koch, mgunduzi wa
vijidudu maradhi aina ya bakteria na tabibu mashuhuri wa Kijerumani
aliyegundua chanzo cha maradhi ya kifua kikuu au TB. Daktari Robert Koch
alianza kutwalii na kufanya utafiti mkubwa juu ya sababu au vyanzo vya
kutokea baadhi ya magonjwa kama vile kipindupindu, kimeta na kifua
kifuu, baada ya kuhitimu masomo yake katika fani ya tiba. Mwaka 1882
Miladia, Robert Koch alifanikiwa kugundua vijidudu maradhi vinavyoitwa
mycobacterium tuberculosis vinavyosababisha kifua kikuu. Ili kukamilisha
uchunguzi wake tabibu huyo Mjerumani alisafiri katika nchi za Afrika
Kusini, Misri na India na kutwalii magonjwa mengineyo maarufu katika
maeneo hayo kama vile Malaria. Mwaka 1905 Robert Koch alitunukiwa Tunzo
ya Nobel katika uwanja wa Tiba.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!