Imethibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie,ambae ni Steve Nyerere, alisema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi ambae ni Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mshtuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!