Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » MWANAMUZIKI DIAMOND WA TANZANIA AVUNJA REKODI YA TUZO ZA MUZIKI ZA TANZANIA ZA KILIMANJARO MUSIC AWARD KWA MWAKA 2014

MWANAMUZIKI DIAMOND WA TANZANIA AVUNJA REKODI YA TUZO ZA MUZIKI ZA TANZANIA ZA KILIMANJARO MUSIC AWARD KWA MWAKA 2014

Written By Unknown on Monday, 5 May 2014 | Monday, May 05, 2014

Tuzo za Muziki za nchini Tanzania zinazodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro (KTMA2014), zilifanyika jumamosi ya tarehe 3 mai katika ukumbi wa Milimani City, jijini Dar es Salaam ambapo Diamond Platinumz aling’aa zaidi na kuweka historia kwa kuondoka na tuzo saba.

Ulikuwa usiku mzuri kwa mwimbaji huyo ambaye alishinda kila kipengele alichokuwa anashindania na hivyo kumfanya aweke historia nzuri katika muziki wake na kuthibitisha kuwa ndiye msanii anayefanya vizuri/anaependwa zaidi nchini humo.
Diamond alishinda tuzo ya Video bora ya mwaka ambayo ni (My Number One), Muimbaji bora wa kiume-Kizazi kipya, mtumbuizaji bora wa kiume –Kizazi kipya, Mtunzi bora wa mwaka – Kizazi Kipya, Wimbo bora wa Afro Pop,  Wimbo bora wa mwaka na Wimbo bora wa kushirikiana alioshirikishwa na rapa Nay wa Mitego (Muziki Gani).

Diamond alipewa kampani mara zote na mchumba wake Wema Sepetu ambaye alikuwa kivutio kwa mashabiki wao kila alipopanda nae jukwaani.
Kwa upande wa hip hop ambao huvuta umakini na msisimko wa watu wengi kutokana na ushindani mkubwa, ulikuwa mzuri mwaka huu kwa rapper wa Mwanza Fid Q ambaye kwa mara ya kwanza alishinda tuzo mbili. Ngosha aliondoka na  tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop na mtunzi bora wa mwaka –hip hop.

Kundi la Weusi lake Joe Majini pia lilibeba tuzo mbili ambazo ni  Kikundi cha Mwaka cha Kizazi Kipya na Wimbo bora wa mwaka ambao (Nje ya Box- Nikki wa Pili feat. Joh Makini &G-Nako).

Rapper mdogo anae julikana kwa jina la Young Killer pia alifanikiwa kuibeba tuzo kwa mara ya kwanza ambapo alishinda tuzo ya Msanii bora anayechipukia.

Kwa upande wa Bendi, mwanamuziki kutoka Mtanzania mwenye asili ya Congo, Christian Bella alikuwa sura mpya katika tuzo hizo mwaka huu na aliondoka na tuzo ya Mtunzi bora wa mwaka.

Tuzo hizo zilipambwa na burudani safi kutoka kwa wasanii mbambali walioonesha uwezo wa hali ya juu ya kutumbuiza; kama Mwana FA, Kundi la Weusi, Vanessa Mdee, Makomando, Madee, Ommy Dimpoz, Diamond, Meninah, Angel, pamoja na bendi za Extra Bongo,Twanga Pepeta na wengine.

Tembelea kwenye ukurasa wetu maridadi wa Facebook wa Ismail Niyonkuru, anza kwa ku Like na utaona picha za matukio ya KTMA 2014.

Angalia orodha kamili ya washindi KTMA2014:
Wimbo bora wa mwaka
Number One – Diamond
Mwimbaji bora wa kike – kizazi kipya
Lady Jaydee
Muimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya
Diamond
Muimbaji bora wa kike taarab
Isha Ramadhan
Muimbaji Bora wa kiume – Taarab
Mzee Yusuf
Muimbaji bora wa kiume – Bendi
Jose Mara
Muimbaji Bora wa Kike – bendi
Luiza Mbutu
Msanii Bora wa Hip Hop
Fid Q
Msanii Bora Chipukizi Anayechipukia
Young Killer
Rapa Bora wa Mwaka – Bendi
Furguson
Mtumbuizaji bora wa kike muziki
Isha Ramadhani
Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki
Diamond
Mtunzi Bora wa Mwaka – Hip Hop
Fid Q
Video Bora ya Mwaka
Number One – Diamond
Bendi ya Mwaka
Mashujaa Band
Kikundi cha Mwaka cha Taarab
Jahazi Modern Taarab
Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya
Weusi
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Taarab
Enrico
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Kizazi kipya
Man Walter
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Bendi
Amoroso
Mtunzi Bora wa Mwaka – Taarab
Mzee Yusuf
Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya
Diamond
Mtunzi Bora wa Mwaka – Bendi
Christian Bella
Wimbo bora wa Kiswahili – Bendi
Ushamba Mzigo – Mashujaa Band
Wimbo bora wa reggae
Niwe na Wewe – Dabo
Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Tubonge – Jose Chameleone
Wimbo bora wa Afro Pop
Number One – Diamond
Wimbo bora wa Taarab
Wasiwasi Wako – Mzee Yusuf
Wimbo bora wa Hip Hop
Nje ya Box – Nick wa Pili f/ Joh Makini & G-Nako
Wimbo Bora wa R&B
Closer – Vanessa Mdee
Wimbo Bora wa Kushirikiana
Muziki Gani – Nay wa Mitego ft Diamond
Wimbo bora wa ragga/dancehall
Nishai – Chibwa f/ Juru
Wimbo bora wa zouk /rhumba
Yahaya – Lady Jaydee
Hall of FAME Award
Hassan Rehani Bichuka
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi