Li Keqiang Waziri Mkuu wa China amesema kuwa, Peking haina nia ya 
kuyakoloni mataifa ya Afrika. Akizungumza na waandishi wa habari jana 
kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika nchi nne za Kiafrika, Li 
Keqiang ameongeza kuwa, lengo kuu la safari yake ni kuongeza kiwango cha
 ubadilishanaji biashara kati ya China na nchi za Kiafrika. Keqiang 
ameyataka mashirika yanayowekeza barani Afrika kuheshimu na kutekeleza 
sheria za nchi walizoko sanjari na kuunga mkono maslahi ya nchi hizo. 
Waziri Mkuu wa China amesema kuwa kiwango cha ubadilishanaji biashara 
kati ya China na nchi za Kiafrika ulifikia kiwango cha dola bilioni 200,
 na kusisitiza kwamba kiwango hicho kinapasa kunyanyuliwa zaidi kwani 
bado kiko chini. Waziri Mkuu wa China amesema kuwa, nchi hiyo inafanya 
juhudi ya kuitisha mikutano mbalimbali na nchi za Kiafrika kwa lengo la 
kuondoa migogoro iliyoko barani humo.Waziri Mkuu wa China ameianza 
safari yake kwa kuitembelea Ethiopia kisha ataelekea Nigeria, Angola na 
siku ya Ijumaa anatarajiwa kuwasili Nairobi mji mkuu wa Kenya.
Home »
siasa kimataifa
 » WAZIRI MKUU WA CHINA AKANA UVUMI WAKUWA NCHI YAKE INAO MPANGO WAKULIKOLINI BARA LA AFRICA
WAZIRI MKUU WA CHINA AKANA UVUMI WAKUWA NCHI YAKE INAO MPANGO WAKULIKOLINI BARA LA AFRICA
Written By Unknown on Monday, 5 May 2014 | Monday, May 05, 2014
Labels:
siasa kimataifa



0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!