Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amekiri kwamba serikali ya Abuja haina
uwezo wa kudhamini usalama wa wananchi wa nchi hiyo. Rais Jonathan
amesisitiza kuwa, hivi sasa Nigeria inahitajia msaada kutoka mataifa ya
kigeni kwa lengo la kurejesha amani na utulivu nchini humo. Amesisitiza
kuwa, serikali ya Abuja inafanya mipango ya kuwepo mashirikiano ya
kiusalama na nchi rafiki kama vile China, Ufaransa, Uingereza na
Marekani. Wizara ya Ulinzi ya Nigeria imetangaza kuwatia mbaroni watu
wanane wanaoshukiwa kwa vitendo vya ugaidi. Mara baada ya kujiri
milipuko miwili ya mabomu katika kipindi cha wiki tatu zilizopita na
kusababisha watu wasiopungua 100 kuuawa, Rais Goodluck Jonathan ametoa
amri ya kufungwa shule na ofisi zote za serikali mjini Abuja kuanzia
tarehe 7 hadi 9 za mwezi huu, wakati wa kufanyika mkutano wa Jukwaa la
Kimataifa la Kiuchumi kuhusiana na Afrika.
Home »
siasa afrika
» SOMA KILE ALICHO KISEMA RAIS WA NIGERIA KUHUSIANA NA SWALA USALAMA NCHI MWAKE
SOMA KILE ALICHO KISEMA RAIS WA NIGERIA KUHUSIANA NA SWALA USALAMA NCHI MWAKE
Written By Unknown on Monday, 5 May 2014 | Monday, May 05, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!