Polisi wa Malaysia wanachunguza kama wanamgambo wa al-Shabaab walikuwa
wakitafuta kuanzisha kambi katika nchi za Asia ya Kusini baada ya
mwanamgambo mshukiwa kutoka Somalia kukamatwa, Shirika la Habari la AFP
liliripoti Ijumaa ya (tarehe 9 Mei).
Polisi walisema kuwa siku ya Alhamisi walimuweka kizuizini Msomali mwenye umri wa miaka 34 huko Kuala Lumpur ambaye alikuwa anatafutwa na polisi wa kimataifa, Interpol, kwa madai ya kuhusiana na a-Shabaab.
"Polisi wanachunguza shughuli za mahabusu nchini Malaysia ili kujua kama kuna magaidi wengine wanaohusiana na al-Shabaab ambao wanaweza kuwa mafichoni au kufanya shughuli ambazo zinaweza kuwa na madhara kwa usalama wa nchi ya Malaysia," Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Datuk Seri Mohammed Bakri Zinin alisema.
"Anaashukiwa wa kutenda makosa yanayohusiana na ugaidi na atachunguzwa kwa mujibu wa taratibu za Sheria ya Makosa ya Usalama (Hatua Maalum) ya mwaka 2012," polisi ilisema katika taarifa yake.
Polisi wanaripotiwa kufuatilia watu wengine watano, ambao wengi wao waliingia Malaysia kwa viza ya wanafunzi, lakini vyombo vya habari vya Malaysia vilinukuu vyanzo rasmi vikisema kuwa kesi mbili hizo hazina uhusiano.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!