Safari ya Waziri Mkuu wa China Li Keiqiang huko Kenya hivi karibuni
imetajwa kuwa ni sehemu ya mashindano ya Umoja wa Ulaya na China kuhusu
kujikita nchini Kenya kiuchumi. Kwa mujibu wa makala iliyochapishwa na
gazeti la Standard la mjini Nairobi, kabla ya kikao cha viongozi wa
Afrika na Umoja wa Ulaya mapema mwezi jana mjini Brussels, mkuu wa
Ujumbe wa EU nchini Kenya Lodewijk Briet alipuuzilia mbali ushawishi wa
China nchini Kenya na Afrika kwa ujumla. Alisema pamoja na kuongezeka
ushawishi wa China barani Afrika Umoja wa Ulaya ungali mshirika muhimu
wa maendeleo barani humo. Mwezi mmoja tu baada ya kikao cha Afrika na EU
mjini Brussels waziri mkuu wa China ametemeblea Afrika ambapo
amesisitiza kuwa China ndie mshirika wa kweli wa Afrika. Akiwa safarini
Kenya, Li Keqian ametoa wito kwa wafanya biashara wa Kenya kuuza bidhaa
zao China ili biashara iwe ya pande mbili. Wakuu wa Beijinga wanasema
biashara na miradi ya maendeleo ya China nchini Kenya kama vile
mabarabara, mahospitali n.k ni ya kiwango cha juu na haiwezi
kulinganishwa na ile ya nchi za Magharibi. Hayo yanajiri katika hali
ambayo katika kipindi cha wiki moja ijayo, Umoja wa Ulaya unatazamiwa
kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo uenyekiti wake
wa sasa unashikiliwa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. Pande mbili
zitajadili njia za kuondoa vizingiti kuhusu biashara ya pande mbili. Kwa
msingi huo inaonekana kuna mashindano makubwa baina ya nchi za
Magharibi na China kuhusu kueneza ushawishi nchini Kenya na Afrika kwa
ujumla.
Home »
siasa afrika
» NCHI YA KENYA YAGEUKA KIGOMBEWA KATI YA ULAYA NA CHINAA
NCHI YA KENYA YAGEUKA KIGOMBEWA KATI YA ULAYA NA CHINAA
Written By Unknown on Monday, 12 May 2014 | Monday, May 12, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!