Serikali za China na Kenya zimetiliana saini makubaliano ya ujenzi wa
njia ya reli itakayotoka Mombasa hadi Nairobi, mji mkuu wa nchi hiyo.
Taarifa kutoka Nairobi zinasema kuwa, mradi wa ujenzi wa reli hiyo
utakaoanza mwezi Oktoba mwaka huu na kukamilika baada ya miaka mitatu
na nusu ijayo, utagharimu dola bilioni tatu na milioni mia nane. Benki
ya Exim ya China itagharamia asilimia 90 na serikali ya Kenya
itagharamia asilimia 10 ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa njia hiyo ya
reli hiyo itakayokuwa na urefu wa kilomita 609.
Imeelezwa kuwa, baada ya kumalizika awamu ya kwanza ya ujenzi huo, awamu ya pili itakua ni kuunganisha njia za reli kutoka Nairobi na kuelekea miji mikuu ya Kampala nchini Uganda, Kigali nchini Rwanda, Juba nchini Sudan Kusini na Bujumbura nchini Burundi. Imeelezwa kuwa, utiwaji saini wa makubaliano hayo uliofanyika jana mjini Nairobi na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa China, Marais wa Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Tanzania. China ambayo inahesabiwa kuwa ni nchi ya pili yenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani, inazidi kuimarisha mahusiano na nchi za bara la Afrika.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!