Siku kama ya leo miaka 126
iliyopita, mwafaka na tarehe 7 Mei 1888 Miladia, serikali ya kikoloni ya
Uingereza ilianzisha uvamizi katika ardhi ya Zimbabwe ya sasa. Mipango
ya kuikalia kwa mabavu Zimbabwe ilibuniwa na mwanasiasa na
mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina la Cecile Rhodes, ambaye aliasisi
shirika la Afrika Kusini la Kiingereza nchini humo. Kwa kusaidiwa na
jeshi la Uingereza, Rhodes aliuwa kwa umati maelfu ya raia wazalendo na
kuwakamata mateka wengine wengi, na hivyo kuweza kuidhibiti ardhi yote
ya Zimbabwe na kuipachika jina lake la Rhodesia.
***********************************************************
Miaka 206 iliyopita katika
siku kama ya leo wananchi wa Uhispania walianzisha harakati dhidi ya
vikosi vya jeshi la Mfalme Napoleon wa Ufaransa, vilivyokuwa vinakalia
kwa mabavu nchi yao. Wakati huo Uhispania pia ilikuwa ikihesabiwa kuwa
miongoni mwa wakoloni wakubwa wa Ulaya na ilikuwa ikikalia kwa mabavu
ardhi nyingi nje ya bara hilo. Baada ya miaka mitano ya mapambano dhidi
ya vikosi vamizi vya Ufaransa, wananchi wa Uhispania walifanikiwa
kuvifukuza vikosi hivyo mwezi Disemba mwaka 1813 kutoka nchini kwao.
***********************************************************
Na siku kama ya leo miaka
1130 iliyopita alizaliwa Ibn Tarara mpokezi wa hadithi na mwandishi wa
Kiislamu huko Iraq. Msomi huyo wa Kiislamu aliandika vitabu vingi katika
uwanja wa fiqhi. Hata hivyo hakuna hata kitabu kimoja miongoni mwa
hivyo kilichobakia hadi hii leo. Vilevile aliandika vitabu katika
taaluma ya fasihi ya lugha ya Kiarabu kikiwemo kile alichokiita "al
Jalisu al Saleh".
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!