Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika nchini Libya, Mundhir al-Raski amesema
kuwa, umoja huo utaunga mkono mikakati yote ya kuirudisha nchi hiyo ya
Kaskazini mwa Afrika kwenye mkondo wa demokrasia. Al-Raski amesema Umoja
wa Afrika umekuwa nyuma ya wananchi wa Libya tangu baada ya mapinduzi
yao dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011. Mwanadiplomasia huyo ameongeza
kuwa, Umoja wa Afrika unasisitiza udharura wa kudhibitiwa silaha
zilizotapakaa huko Libya ili kutoa fursa ya kuimarishwa amani na
utulivu. Mjumbe huyo maalum wa AU nchini Libya amesema nchi za barani
Afrika zitashirikiana na taasisi za kimataifa kama vile Umoja wa
Mataifa, Benki Kuu ya Dunia na Umoja wa Ulaya kuhakikisha kwamba Libya
inarudi katika hali yake ya kawaida na demokrasia inachukua tena nafasi
yake.
Home »
siasa afrika
» UN KUISADIA LIBYA KWENYE HATUWA ZA UREJESHAJI WA DEMOKRASIA
UN KUISADIA LIBYA KWENYE HATUWA ZA UREJESHAJI WA DEMOKRASIA
Written By Unknown on Wednesday, 7 May 2014 | Wednesday, May 07, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!