Shirika la Msamaha Duniani Amnesty
International limesema kuwa, vikosi vya serikali na waasi wa Sudan
Kusini wanafanya ukatili wa kutisha dhidi ya binadamu. Katika ripoti
yake iliyotolewa leo, shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema,
askari watiifu kwa Rais Salva Kiir na wanamgambo watiifu kwa Riek
Machar wanawalenga raia kwa makusudi katika vijiji na miji na hata
maeneo ya Umoja wa Mataifa.
Michele Kaari Naibu Mkurugenzi wa
Amnesty International barani Afrika amesema kuwa, pande zote hizo mbili
zimekiuka sheria nyingi za kimataifa za haki za binadamu na utu. Shirika
hilo limesema kuwa, wachunguzi wake mwezi Machi waligundua makumi ya
makaburi ya umati yakiwemo matatu katika mji wa Bor kaskazini mwa Sudan
Kusini.
Hata hivyo msemaji wa jeshi la Sudan
Kusini Philip Anguer amesema kuwa vikosi vya serikali vimekuwa vikifuata
sheria ipasavyo na kwamba yeyote atakayetenda jinai atatiwa mbaroni.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!