Mahakama ya Uingereza imemtuhumu James Stuart Hall mwendesha vipindi wa
zamani wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC kuwa aliwabaka na
kuwadhalilisha kijinsia wasichana wawili katika muongo wa 1970. Taarifa
iliyotolewa na Mahakama ya Uingereza hapo jana inaeleza kuwa,kabla ya
kuwabaka wasichana hao waliokuwa na umri wa miaka 13 na 14, Stuart
Hall alikuwa akiwanywesha pombe na kisha kuwaingiza kwenye chumba cha
kubadilishia nguo kilichokuwa kwenye studio za BBC mjini Manchester,
Uingereza.
Stuart mwenye umri wa miaka 84 alifikishwa mahakamani kwa mara nyingine tena tarehe 6 Mei akitokea gerezani. Awali Stuart alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela baada ya kupatikana na kosa la kuwanajisi na kuwabaka wasichana 13, wenye umri wa miaka 9 hadi 17 katika kipindi cha miaka ya 1964 hadi 1986. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi Aprili uliopita, mwendesha vipindi huyo wa zamani wa BBC alikiri mahakamani kutenda vitendo hivyo visivyo vya kiakhlaki na kimaadili.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!