Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO kimeunga mkono operesheni zinazofanywa
hivi sasa na majeshi ya nchi hiyo dhidi ya makundi ya waasi. Luteni
Kanali Felix Basse Msemaji wa vikosi vya MONUSCO ameyasema hayo mjini
Goma na kuongeza kuwa, uungaji mkono huo unafanyika huku vikosi vya
umoja huo vikiendelea kufanya doria mbalimbali katika maeneo ya Bohuma,
Bukiringi na Borasi.
Luteni Kanali Basse ameongeza kuwa, operesheni hiyo inafanywa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kutoka nchi za Guatemala na Bangladesh. Msemaji wa MONUSCO nchini Kongo amefafanua kuwa, operesheni ya doria inafanyika kwa lengo la kuzuia uwezekano wa kutokea shambulio la kushtukiza la makundi ya waasi sanjari na kulinda maisha ya raia katika eneo la Tshabi.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, eneo la mashariki mwa Kongo limekuwa likikabiliwa na machafuko yanayosababishwa na makundi ya waasi ambapo inasemekana kuwa makundi hayo yanapata uungaji mkono wa serikali za Uganda na Rwanda, tuhuma ambazo zimekadhibishwa mara kadhaa na serikali za Kigali na Kampala.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!