Syria imelikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa
kudharau tahadhari za mara kwa mara kwamba magaidi wanaoungwa mkono na
madola ya kigeni wana silaha za mauaji ya umati. Bashar al Jaafari
mwakilishi wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema, Damascus
imewatahadharisha maafisa wa umoja huo kwa kuwaandikia barua zaidi ya
100 kuhusu hatari hiyo. Pia amezikosoa baadhi ya nchi wanachama wa
Baraza la Usalama kwa kuyasaidia makundi ya kigaidi nchini Syria kupata
silaha za mauaji ya umati .
Wakati huo huo kiongozi wa kundi kubwa zaidi la wapinzani wa Syria wanaoungwa mkono na nchi za kigeni ameitaka Marekani iwapatie silaha zaidi kwa ajili ya kupigana na serikali ya Damascus. Ahmad Jurba mkuu wa muungano unaojiita Syrian National Coalition (SNC) alitoa ombi hilo nchini Marekani na kudai kuwa, wapiganaji wake wanahitajia silaha bora zaidi ili waweze kubadilisha mlingano wa nguvu nchini Syria.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!