Umoja wa Mataifa umeitaka nchi ya Qatar kuondoa mfumo wa uwakala
unaowatia pingu wafanyakazi wa kigeni na kuwabana wasiweze kuondoka kwa
waajiri wao.Wawakilishi wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa
Mataifa wameelezea wasiwasi wao kuhusu kunyonywa wafanyakazi wa kigeni
wanaofanya kazi chini ya sheria za uajiri za hivi sasa nchini Qatar.
Baraza hilo limesema, serikali ya Doha imeshindwa kuweka sheria nzuri za kazi na kwamba kuna ripoti nyingi zinazoonesha kuweko ukiukwaji mkubwa wa haki za wafanyakazi wa kigeni, hasa wanaofanya kazi za kutayarisha mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia la Soka za mwaka 2022.
Ripoti iliyotolewa mwezi Aprili na Amnesty International ilieleza kuwa, wafanyakazi wa kigeni katika nchi hiyo ya Kiarabu wananyanyaswa kwa namna mbalimbali kama vile kulazimishwa kufanya kazi kwa muda mrefu, kutukanwa na hata kudhalilishwa kimwili na kijinsia.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!