Umoja wa Mataifa umezituhumu pande zinazohasimiana nchini Sudan
Kusini kwamba zimetenda jinai dhidi ya binadamu katika kipindi cha miezi
5 ya mapigano. Ripoti mpya ya UN iliyotolewa hapo jana imetaka
uchunguzi ufanywe ili kubaini waliokiuka haki za binadamu na kuvunja
sheria za kimataifa. Aidha ripoti hiyo yenye kurasa 62 imependekeza
kuchukuliwa hatua za haraka kuwalinda raia wasio na hatia nchini Sudan
Kusini. Katika kalibu hiyo, ripoti imependekeza kutumwa askari zaidi wa
kulinda amani wa Umoja wa Mataifa sambamba na kupewa nguvu zaidi za
kukabiliana na hujuma dhidi yao na raia.
Huku hayo yakijiri, habari zinasema kuwa, kiongozi wa waasi, Riek Machar, amewasili mjini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mazungumzo ya ana kwa ana na Rais Salva Kiir lengo likiwa ni kutatua mgogoro unaoendelea Sudan Kusini.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!