Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC)
amedokeza kuwa huenda korti hiyo ikatoa waranti wa kukamatwa viongozi
waandamizi wa kundi la Boko Haram kutokana na kuwateka nyara wanafunzi
wa kike zaidi ya 200 kaskazini mwa Nigeria. Bi. Fatou Bensouda amesema
kitendo cha wakawanamgambo wa Boko Haram cha kuwateka nyara wasichana wa
kike nchini Nigeria kinahesabiwa kuwa jinai dhidi ya binadamu.
Bensouda amesema jinai walizofanya wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria zimekuwa zikinyamaziwa lakini kadhia ya kutekwa nyara wanafunzi wa kike zaidi ya 200 haiwezi kunyamaziwa kamwe. Mwanasheria huyo amewaonya wanamgambo wa Boko Haram dhidi ya kuchukua hatua ya kuwauza wasichana hao akisema hilo litatia msumari wa moto kwenye kidonda.
Hii ni katika hali ambayo, Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amesema kuwa, oparesheni kali zimeanza kwa lengo la kuwatafuta na kuwaokoa wanafunzi wa kike waliotekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram mwezi uliopita.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!