Klabu ya Arsenal imerudi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England
kufuatia ushindi wa bao 1-0 jioni ya jana dhidi ya West Brom kwenye Uwanja wa
Emirates,jijini London.
Na
kwa kipigo cha Everton juzi kutoka kwa Manchester City, The Gunners
tayari wamejihakikishia kucheza kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Olivier Giroud alifunga bao hilo pekee dakika ya 14 likiwa la 22 msimu huu, Arsenal
ikiibuka na mabadiliko makubwa katika kikosi cha kwanza kutoka kile
kilichofungwa na Newcastle Jumatatu, Mathieu Flamini akichukua nafasi ya
Aaron Ramsey, ambaye alipumzishwa kwa sababu majeruhi.
Arsenal
sasa inatimiza pointi 76 baada ya kucheza mechi 37 na inaendelea kubaki
nafasi ya nne nyuma ya Chelsea yenye pointi 79 za mechi 37, Manchester
City pointi 80 za mechi 36 na Liverpool pointi 80 za mechi 36 pia.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!