Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » WA MISRI LEO WAINGIA KWENYE SIKU YAO YA 2 YA UCHAGUZI WA RAIS MPYA BAADA YA MORSI.

WA MISRI LEO WAINGIA KWENYE SIKU YAO YA 2 YA UCHAGUZI WA RAIS MPYA BAADA YA MORSI.

Written By Unknown on Tuesday, 27 May 2014 | Tuesday, May 27, 2014

Wananchi wa Misri,jana Jumatatu na hii leo Jumanne wanapiga kura kuchagua rais mpya, kwenye uchaguzi ambao aliyekuwa mkuu wa majeshi wa nchi hiyo, Jenerali Abdel Fatah al-Sisi anatarajiwa kushinda.
 Al-Sisi anapewa nafasi kubwa ya kushinda kwenye uchaguzi wa mwaka huu kutokana na kuwa na uungwaji mkono karibu nchi nzima kufuatia mapinduzi aliyoyaongoza ya kumuondoa madarakani Mohamed Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood.

Jenerali Sisi anatarajiwa kumsinda mpinzani wake wa karibu anayepewa nafasi ya kutoa upinzani kwa kiongozi huyo, Hamdeen Sabbahi ambaye kwenye uchaguzi uliopita alikuwa mshindi wa tatu.
Mamia ya wananchi wa Misri wameonekana wakiwa kwenye misururu mirefu ya watu wakisubiri kufunguliwa na kisha kuanza kupiga kura kwenye vituo mbalimbali vilivyoko nchi nzima.
Al-Sisi mwenyewe amepiga kura kwenye kituo cha Heliopolis ambako alikutana na mamia ya wafuasi wake wanaomuunga mkono na kuanza kumzonga wakati akipiga kura yake.
Mji wa Cairo kwa mara ya kwanza ukilinganisha na uchaguzi uliopita umeshuhudia maelfu ya wananchi wakijitokeza kwenye vituo vya kupigia kura mapema zaidi licha ya hofu ya kiusalama ambayo imekuwepo katika mji huo hivi karibuni.
Sisi mwenyewe wakati wa kampeni zake aliahidi kuwa iwapo ataingia madarakani atahakikishakuwa analeta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwenye taifa hilo ambalo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imekuwa vigumu kusimama kiuchumi.
Kwa upande wake, Hamdeen Sabbahi ambaye amekuwa mshirika wa karibu wa Serikali ya Syria, amesema kuwa atahakikisha kunakuwa na usawa nchini humo pamoja na kumaliza utawala wa kijeshi ambao yeye mwenyewe aliunga mkono wakati rais Morsi akiondolewa madarakani.
Kwenye uchaguzi wa mwaka huu kilichokuwa chama kikuu cha upinzani chenye nguvu cha Muslim Brotherhood kimepigwa marufuku kushiriki kwenye uchaguzi wa mwaka huu baada ya kudaiwa kuhusika na makundi ya kigaidi nchini humo.
Uchaguzi huu unatarajiwa kumaliza miaka mitatu ya mzozo wa kisiasa nchini humo toka rais Morsi alipoangushwa madarakani ambapo kumekuwa na hali ya sintofahamu kuhusu suala la demokrasia nchini humo.
Wananchi wa taifa hili wanashiriki uchaguzi huu huku kukiwa na kumbukumbu ya kuuawa kwa wafuasi zaidi ya 1400 wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohamed Morsi ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini na kuchochea machafuko nchini humo.
Hata hivyo mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo yanasema kuwa licha ya mapinduzi yaliyofanyika bado nchi hiyo itasimama kidemokrasia na kwamba hivi sasa maisha ni mazuri zaidi ukilinganisha na hali ilivyokuwa wakati wa utawala wa Hosni Mubarack.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi