Ripoti zinasema kuwa mapigano baina ya askari wa nchi hizo mbili yalianza tena jana kwenye eneo la mpakani. Rwanda na Congo zinatuhumiana kwa kusababisha machafuko hayo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda ambaye pia ni msemaji wa serikali ya nchi hiyo Louise Mushikiwabo amesema machafuko hayo ya mpakani yanakwamisha juhudi za kurejesha amani, utulivu na maendeleo kwa raia wa nchi hizo mbili.
Uhusiano wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umekuwa matatani tangu baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Rwanda imekuwa ikituma majeshi yake katika ardhi ya Congo ikidai kuwa inawasaka waasi wa Kihutu wa Interahamwe ambao walihusika na mauji hayo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!