Mapigano yanayoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baina ya
wanamgambo wa Kikristo na wapiganaji wa Kiislamu yamesababisha vifo vya
watu wasiopungua 22.
Mapigano hayo yaliripotiwa kuanza jana Alkhamisi mashariki mwa nchi hiyo baada ya wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka kuua Waislamu wawili. 21 kati ya wahanga wa mapigano hayo waliuawa katika mji wa Bambari na kijiji cha Liwa. Vilevile nyumba 100 zimechomwa moto katika machafuko hayo.
Mapigano ya sasa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yamenza tena baada ya serikali ya nchi hiyo kuiomba Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ifanye uchunguzi juu ya uhalifu uliofanyika nchini humo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Wapiganaji wa Kikristo wa kundi la Anti Balaka wanatuhumiwa kutenda mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu walio wachache katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!