Klabu ya Arsenal,
imekunja kitita cha paundi milioni 5.6 kutokana na mauzo ya kiungo wao
wa zamani Cesc Fabregas kwenda Chelsea. Kiungo huyo wa kimataifa wa
Hispania alikamilisha usajili wake huo wa kurudi London jana kwa ada ya
paundi milioni 30 akitokea Barcelona, mkataba mabao utamuwezesha kulipwa
kitita cha paundi 150,000 kwa wiki.
Lakini dili hilo litazidi kuutunisha mfuko wa usajili wa Arsenal ambao tayari umetengewa paundi milioni 100 na kuwawezesha kuanza mazungumzo ya kumsajili Mario Balotelli ambao ni mmoja kati wachezaji wanaowindwa na meneja Arsene Wenger katika usajili wa majira haya ya kiangazi. Kwa kuongeza, Arsenal pia inaaminika kuweka dili lingine la kupata asilimia 50 ya faida kutoka kwa Fabregas kama akiamua kuondoka tena Chelsea. Hivyo pamoja na Arsenal kushindwa kumsajili tena nahodha wao huyo wa zamani lakini bado wameendelea kunufaika na mauzo yake kwa mahasimu wao hao wa jiji la London.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!