
Ila vile wengi walikuwa wakisubiria wala si vile ilivyo tokea,kwenye defenda ya Usuisi iliyo kuwa imeshikiliwa na Philippe Senderos na Mkongwe Johan Djourou iliweza kutepeteshwa vibaya na washambuliaji mahiri kama vile Valbuena mfupi kuliko wote akina Karimu Benzema na bila kuwasahau akina Sissokho.
Ufaransa iliwakaba kwenye koo wa Suisi mwanzo hadi mwisho nakuondoka wakimezeshwa ma bao ma 5 huku tukiitowa penalti ambayo benzema aliyo shindwa na lile la 6 ambalo liliingizwa huku refa akiwa amesha puliza kipenga kuwa muda umekwisha ilikuwa ni kwenye muda wa ziada,Huku Usuisi wakijipachikia ma bao mawili waliyo fungwa wafaransa kwa uzembe wao wenyewe moja wapo nilile la ukuta feki uliyo wekwa na pindi ilipo pigwa shuti mchezaji Sissokho aliupisha mpira na kipa wa Ufaransa Loris kuukuta tayari upo wavuni.
Ufaransa inasaliya na match moja tu ili imalize huyu mzunguuko wa kwanza ambao imesha uvuka ambapo imeuvuka kwa kujizolea pointi 6 chini ya 9 na ikisaliya na huyo mchezo umoja na kama itaufunga itakuwa imekamilisha pointi 9 chini ya 9.

Inasemekana Varane anasumbuliwa na Estomac ambayo itampelekea kukaa nje huku nafasi yake ikichukuliwa na mchezaji wa Club ya Arsenal Laurent Koscielny,japo nafasi yake itakuwa ngumu kuzibika pengo la Varane ila kwenye mzunguuko wa pili ataweza kurejea kwenye nafasi yake yani anapumzishwa kwa mechi hiyo akiisubiria ya kufwatia ya kwenye mzunguuko wa pili.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!