Mshambuliajii nyota wa AC
Milan na timu ya taifa ya Italia, Mario Balotelli anakabiliwa na
changamoto ya kuwa fiti kabla ya mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia
kutokana na kusumbuliwa na majeraha madogo ya msuli. Nyota huyo mwenye
umri wa miaka 23 anatarajiwa kuwa mchezaji muhimu katika mpango ya kocha
Cesar Prandelli kwa ajili ya michuano hiyo baadae mwezi huu haswa
kutokana na kuenguliwa kwa Giuseppe Rossi katika kikosi hicho. Mkongwe
Antonio Cassano na washambuliaji Alessio Cerci, Ciro Immobile na Lorenzo
Insigne ndio wanatarajiwa kuwa mbadala katika safu ya ushambuliaji kama
Balotelli hatakuwa fiti kwa asilimia mia moja. Kocha wa Italia Enrico
Castlellaci amebainisha kuwa nyota huyo wa zamani wa Manchester City
alipata majeraha ya msuli wakati akiwa kambini na timu hiyo huko
Coverciano hivyo kumaanisha anaweza kukosa mechi ya ufunguzi dhidi ya
Uingereza itakayochezwa huko Manaus Juni 14 mwaka huu.
Home »
michezo ulaya
» HILI NDILO TATIZO AMBALO LINAMKABILI BALOTELLI NA HUENDAA AKAIKOSA MECHI YAO YA KWANZA YA UFUNGUZI WA KOMBE LA DUNIA
HILI NDILO TATIZO AMBALO LINAMKABILI BALOTELLI NA HUENDAA AKAIKOSA MECHI YAO YA KWANZA YA UFUNGUZI WA KOMBE LA DUNIA
Written By Unknown on Monday, 2 June 2014 | Monday, June 02, 2014
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!