Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » KAMA ULIKUWA HAUJUI BASI HIZI NDIZO DALILI ZA UGONJWA MBAYA WA ZINAA UITWAO KISONONOO DUUU!!!!

KAMA ULIKUWA HAUJUI BASI HIZI NDIZO DALILI ZA UGONJWA MBAYA WA ZINAA UITWAO KISONONOO DUUU!!!!

Written By Unknown on Friday, 6 June 2014 | Friday, June 06, 2014

Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa, ugonjwa huu hutokana na wadudu aina ya Neisseria gonorrhoeae. Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa tendo la ngono na hata kutoka kwa mama mjamzito anapojifungua huweza kumuambukiza pia mtoto endapo atakuwa alikuwa nao. Ugonjwa wa kisonono kwa mara nyingi huwapata vijana na watu wazima. Waathirika wengi wa ugonjwa huu wa kisonono huambatana na magonjwa mengine ya zinaa, kwasababu kunabaadhi ya magonjwa mengine ya zinaa hujificha bila kuonyesha dalili, hivyo kukuta ukiugulia ndani kwa ndani. Ugonjwa wa kisonono, unazuilika na kutibika pia, unaposikia dalili zozote za magonjwa ya zinaa, unashauriwa kumchukua mwenzi wakona kuwahi hospitali  kuchukua vipimo kwaajili ya matibabu.

NA HIZI NDIZO DALILI ZA UGONJWA HUO WA KISONONO.

Mara nyingi ugonjwa wa kisosnono huwa hauonyeshi dalili yoyote mwanzoni. Lakini ukionyesha dalili basi kwa mwanaume utasikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuambatana na usaha kutoka uumeni, kwa mwanamke pia dalili ni hizo hizo - maumivu wakati wa haja ndogo na kutoa usaha ukeni.Usaha huo unaotoka uumeni au ukeni, huwa mzito na rangi ya kijani-njano, ambapo kwa mwanaume anaweza kuhisi maumivu katika korodani zake. Kwa Wanawake maumivu yanaweza  kuwa chini ya tumbo, uchungu wakati wa ngono, na damu Isiyokuwa ya kawaida kutoka kwenye uke.

 Kama kisonono huenda kikakaa kwa muda mrefu mwilini  bila kutibiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi ya afya. Katika wanaume, inaweza kusababisha makovu ndani ya njia ya mkojo, ambayo inaweza kusababisha maumivu wakati wa kukojoa.
Katika wanawake, kisonono kinaweza kusababisha zaidi kutoka eneo la uke na kusababisha papo hapo ugonjwa mwingine wa "pelvic inflammatory" (PID) - maambukizi katika maeneo mbali mbali ya uzazi yanaweza kusababisha utasa.
 
Katika wanaume na wanawake, kisonono  kisichotibika kwa muda muafaka, huenda huweza kuenea kupitia damu katika sehemu za mwili ambazo ni mbali na viungo vya uzazi, na kusababisha uvimbe katika viungo, ngozi, mifupa, tendons, moyo, au hata eneo karibu na ini.


Natumai umepata elimu na ninahakika utatumia ushauri huu kwa watu unaofahamu kuwa wanatatizo kama hili. Asanteni!
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi