Dunia inasurprises nyingi, kuna watu hawapendi muonekano wao na
hufanya juu chini hata kufanya upasuaji ili wawe na sura ya mvuto lakini
wapo wengine ambao hawapendi kabisa jinsia waliyopewa na Mungu.
Mtoto
wa mfalme wa R&B, Robert Kelly aliyezaa na muigizaji Andrea Kelly
aliyewahi kuwa mke wake ameipinga jinsia yake na kujiunga na kundi la
watu wanaoishi kwa mtazamo tofauti na jinsia zao na kujibadilisha kuwa
jinsia tofauti japo sio kwa kubadili viungo vya uzazi (Transgender/FTM).Mtoto huyo wa kike mwenye umri wa miaka 14 anaefahamika kwa jina la Jaya Kelly, hivi sasa anaitwa Jay Kelly na anaonekana kujuta kuzaliwa msichana.
Hata hivyo, ameona bado hajachelewa na amebadili muonekano na aina ya
maisha yake. Jay Kelly ni miongoni mwa watoto watatu wa R Kelyy aliozaa
na Andrea. Wengine ni Joann Kelly na Robert Kelly Jr.
Huu ni muonekano wa sasa wa Jaya aka Jay:
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!