Siku kama ya leo miaka 1409 iliyopita
yaani tarehe 4 Shaaban mwaka 26 Hijria, alizaliwa Abbas bin Ali bin Abi
Talib mashuhuri kwa lakabu ya Abul Fadhl. Mama yake ni Ummul Baniina,
ambaye aliolewa na Imam Ali (A.S) baada ya kufariki dunia bibi Fatima
Zahra AS. Abbas alifahamika mno kutokana na elimu, ukweli na uchaji
Mungu wake. Kutabahari kwake kielimu kuliwafanya watu wengi kumrejea kwa
ajili ya kutatuliwa masiala mbalimbali ya kielimu.
-----------------------------------------------------------------------------
Miaka 14 iliyopita katika siku kama ya
leo,sawa na tarehe 12 Khordad mwaka 1379 Hijiria Shamsia, aliuawa
Hujjatul Islam Sayyid Ali Akbar Abuturabi, mwanzuoni mwenye mwamko na
mwanaharakati wa Iran katika ajali ya gari pamoja na baba yake Ayatullah
Sayyid Abbas Abuturabi. Hujjatul Islam Sayyid Ali Akbar Abuturabi
alizaliwa mwaka 1318, kwa mujibu wa kalenda ya Iran, katika mji wa
kidini wa Qum. Alijifunza elimu ya dini kutoka kwa maulamama wakubwa
akiwemo Imam Khomeini (M.A). Hujjatul Islam Abuturabi katika mapambano
ya kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu mara kadhaa alikamatwa na kuteswa na
vibaraka wa Shah. Wakati vya vita vya Iran na Iraq mwaka 1359 alikamatwa
mateka na askari wa utawala wa Baath wa Iraq na kufungwa kwa miaka 10
katika jela zenye mateso makali za Iraq. Lakini alivumilia kiasi cha
kuwa mashuhuri miongoni mwa mateka wa Iran kwenye jela hizo.
Alipoachiliwa huru aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa
Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya mateka na walioachiliwa huru.
-------------------------------------------------------------------------------
Na miaka 132 iliyopita kama leo,
alifariki dunia Giuseppe Garibaldi kamanda mzalendo na kiongozi wa
harakati ya kuleta umoja wa Italia. Giuseppe alizaliwa mwaka 180 na
wakati wa ujana wake alifanya kazi mbalimbali na mwishowe kujiunga na
jeshi. Baadaye alichaguliwa kuwa kamanda wa wanaharakati wa kupigania
uhuru wa Italia na alifanya jitihada nyingi za kuleta umoja nchini humo.
Kwa ajili hiyo alijulikana katika historia ya Italia kama shujaa wa
taifa.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!