Mchezaji mahiri wa Real Madrid mreno Cristiano Ronaldo, ana siku mbili za kupiga tizi la
maana kabla ya kuiongoza Ureno kwenye mchezo wao wa kwanza wa Kombe la
Dunia dhidi ya Ujerumani utakaopigwa hii leo Jumatatu saa 12:00 usiku yani (18h) majira ya Bujumbura.
Lakini, wakati staa huyo wa Real Madrid akijipanga
asiangukie pua uwanjani, mambo yamekwenda kombo nje ya uwanja baada ya
kuzidiwa na bondia Floyd Mayweather Jr kwenye kinyang’anyiro cha
mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani.
Mayweather, ambaye ni bondia mwenye hadhi kubwa
kwenye mchezo huo wa ngumi, ametajwa kuwa kinara kwenye takwimu za
Jarida la Forbes na hivyo kumporomosha Ronaldo, ambaye akili yake yote
kwa sasa ipo kwenye kujenga hadhi yake katika Kombe la Dunia baada ya
kushuhudia Neymar akitengeneza heshima juzi Alhamisi.
Kwenye ligi ya mwanamichezo anayelipwa pesa
nyingi, Mayweather anamiliki utajiri wa Dola 105 milioni, wakati Ronaldo
utajiri wake ni Dola 80 milioni.
Kwenye orodha ya wanamichezo watano wanaolipwa pesa nyingi inawahusisha pia wakali LeBron James, Lionel Messi na Kobe Bryant.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!