Mapenzi
yaliyopitiliza ya shabiki wa muziki wa Marehemu Whitney Houston
yamemfanya kununua nyumba ya mwanamuziki huyo na kuahidi kuitunza kwa
ajili yake.Mapenzi yaliyopitiliza ya shabiki wa muziki wa Marehemu Whitney Houston yamemfanya kununua nyumba ya mwanamuziki huyo na kuahidi
kuitunza kwa ajili yake.Nyumba hiyo ya Whitney iliyopo katika
mji wa Mendham huko New Jersey imeuzwa kwa takribani dola milioni 1.5
kwa Matthew Krauthamer, ambaye ni shabiki wake na amedai kuwa hataki
kuibadilisha nyumba hiyo yenye ukubwa wa hekari tano.
Nyumba hiyo
ambayo Whitney hakuishi kwa muda wa miaka mitano kabla ya kifo chake
kilichohusishwa na dawa za kulevya kilichotokea February mwaka 2012 ina
jumla ya vyumba vitano, garage sita za magari.Wakati
mwanamuziki huyo ananunua nyumba hiyo aliiongezea studio ya kurekodi
muziki, chumba cha michezo, chumba cha burudani, uwanja wa mchezo wa
Tennis na nyumba ya bwawa la kuogelea na mmiliki huyo mpya amesema
anataka kuifanya nyumba hiyo ya kiburudani zaidi.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!