Siku kama ya leo miaka 24 iliyopita sawa na tarehe 16 Khordad 1368
Hijria Shamsia, mamilioni ya wananchi wa Iran waliojawa na huzuni kubwa
waliuzika mwili mtoharifu wa Imam Khomeini MA karibu na makaburi ya
mashahidi wa vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran ya Kiislamu,
ya Behesht az-Zahra (AS), pambizoni mwa mji wa Tehran. Zaidi ya wananchi
na Waislamu milioni kumi kutoka miji mbalimbali nchini Iran pamoja na
nje ya nchi walishiriki kwenye mazishi hayo. Kwa hakika mazishi hayo
adhimu yalikuwa medani ya Kihirisho la namna ambayo watu wa Iran na
hata watu kutoka maeneo mengine ya dunia walivyo watiifu kwa kwa njia
ya Imam na Mapinduzi ya Kiislamu.
Siku kama ya leo miaka 32 iliyopita, muwafaka na tarehe 6 Juni 1982, utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine tena ulianzisha mashambulizi dhidi ya ardhi ya Lebanon. Majeshi ya Israel yalianzisha mashambulizi hayo kwa kisingizio cha kudhamini usalama wake huko kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, kwa kuuteka mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
Miaka 874 iliyopita katika siku kama ya leo yaani tarehe nane Shaaban
mwaka 561 Hijria Qamaria alizaliwa Ahmad bin Muhammad bin Mufarraj bin
Ani al-Khalil maarufu kama Abu al-Abbas al-Nabat au Ibnal-Rumiyah
Mwislamu mwandishi hadithi, mwanasayansi mtaalamu wa mimea au botania
mtaalamu wa dawa au mfamasi ambaye alizaliwa huko Andalusia katika
Hispania ya leo. Alianzia masomo yake huko Andalusia na kisha akasafiri
kuelekea katika nchi kadhaa kutafuta elimu zikiwemo nchi za Afrika
Kaskazini na Iraq. Mbali na masomo ya kisayansi hakughafilika pia na
masomo ya kidini hasa Hadithi. Ibn Rumiya ameandika vitabu vingi kuhusu
botania, fiqhi na hadithi. Baadhi ya vitabu vyake vilipotea lakini
vingine vingi alivyoandika kwa lugha ya Kiarabu bado vingali vinatumiwa
na watafiti. Kati ya wanafunzi wake ni mwanabotania mwingine maarufu wa
Andalusia, Ibn al-Baitar.
------------------------------------------------------------
Siku kama ya leo miaka 32 iliyopita, muwafaka na tarehe 6 Juni 1982, utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine tena ulianzisha mashambulizi dhidi ya ardhi ya Lebanon. Majeshi ya Israel yalianzisha mashambulizi hayo kwa kisingizio cha kudhamini usalama wake huko kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, kwa kuuteka mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
------------------------------------------------------------
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!