Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KUNDI LA BOKO HARAMU LIMEFANYA TENA UWARAMU WAO KWA KUWAUWA MAMIA YA WATU HUKO BORNO KASKAZINI MWA NIGERIA

KUNDI LA BOKO HARAMU LIMEFANYA TENA UWARAMU WAO KWA KUWAUWA MAMIA YA WATU HUKO BORNO KASKAZINI MWA NIGERIA

Written By Unknown on Friday, 6 June 2014 | Friday, June 06, 2014

Mamia ya watu wanahofiwa kupoteza maisha kufuatia hujuma ya magaidi wa kundi la Boko Haram katika vijiji vinne kaskazini mwa Nigeria.
Baadhi ya viongozi wa kijamii wamesema watu 400 hadi 500 wameuawa Jumanne wiki hii katika hujuma ya kundi la kitakfiri la Boko Haram dhidi ya wilaya ya Gwoza katika jimbo la Borno. Habari hizo bado hazijaweza kuthibitishwa kutokana na mawasiliano duni katika eneo hilo. Iwapo habari hizo zitathibitika kuwa za kweli, basi hujuma hiyo itahesabiwa kuwa mbaya zaidi katika miaka mitano ya uasi wa Boko Haram nchini Nigeria.
Vijiji vilivyoshambuliwa ni vya Goshe, Attagara, Agapalwa na Aganjara na imedokezwa kuwa magaidi wa Boko Haram wamechukua udhibiti wa vijiji hivyo vyote huku wakaazi walionusurika wakitoroka kutokana na vikosi vya usalama kushindwa kufika katika eneo hilo.  Siku ya Jumatano pia magaidi wa Boko Haram waliua watu 45 katika kijiji cha Barderi karibu na Maiduguri, mji mkuu wa Jimbo la Borno ambalo ni ngome kuu ya magaidi hao.
Wanamgambo wa Boko Haram wangali wanawashikilia mateka wasichana wa shule wapatao 223 waliotekwa nyara hivi karibuni katika jimbo hilo Borno. Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi