Rais aliyepinduliwa na jeshi nchini Misri Muhammad Morsi amewataka wananchi waaendelee kuandamana na kupinga serikali mpya ya nchi hiyo. Kupitia ujumbe wake aliotuma kutoka jela, Morsi amewataka Wamisri waendeleze maandamano ya mapinduzi ya amani dhidi ya serikali inayoungwa mkono na jeshi akisema kuwa, mapinduzi yatashinda hivi karibuni huko Misri.
Pia Morsi amekiri kuwa alifanya baadhi ya makosa alipokuwa madarakani lakini hata hivyo amesema hakuwafanyia khiyana Wamisri na kuahidi kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi na jinai nchini humo.
Ujumbe huo umetolewa ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa rasmi Abdul Fattah al Sisi mkuu wa jeshi wa zamani wa Misri kuwa rais wa nchi hiyo, baada ya tume ya uchaguzi kutangaza kuwa ameshinda uchaguzi kwa asilimia 96.91 katika uchaguzi uliosusiwa na makundi mengi ya kisiasa ya Misri huku wanachi wakijitokeza kwa kiasi kidogo sana katika upigaji kura.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!